Katedrali-Basilika Bikira Maria wa Pilar- Zaragoza

Bikira wa Pilar

Mnamo Januari 2, mwaka 40, ukingoni mwa Mto Ebro, Bikira Maria, ambaye bado alikuwa anaishi Palestina, alikuja Zaragoza katika mwili wake halisi ili kumfariji mtume Yakobo, aliyesindikizwa na kikundi kidogo cha waongofu, waliokuwa wamehubiri siku nzima. Maria aliwaachia nguzo ya yaspi ambapo Wakristo wa karne ya kwanza walijenga, kama ukumbusho, kanisa dogo ambalo limepanuliwa na kurekebishwa kwa karne nyingi.

Wanasema kwamba Papa (Mtakatifu Yohane Paulo II) alipokuja kwenye Hekalu hili alisema: “Jinsi ulivyo mdogo, lakini una mvuto mkubwa kama nini!”

Bikira anapenda kuwa mdogo, mnyenyekevu, aliyefichwa.

Kiko Argüello

Mungu alikuwa amepanga tuje hapa, katika uwanja huu ambapo Basilika ya Maria wa Pilar ipo, ikiwa mojawapo ya Basilika kubwa zaidi nchini Hispania. Bikira wa Pilar ni mtakatifu somo wa Hispania na mtaona hapa picha ya Bikira juu ya nguzo, kwa sababu Pilar inamaanisha nguzo.

Kiko kwenye mkutano wa miito huko Zaragoza mnamo 1989

Mapokeo ya zamani zaidi yanasema kwamba wakati Yakobo alikuja kuhubiri Hispania (kwa sababu Roho Mtakatifu alimchukua hadi “Finisterrae”, hadi miisho ya dunia, kama Maandiko yanavyosema), alikuja akisindikizwa na makatekista wasafiri, mitume wengine ambao huko Zaragoza wanaitwa “wanaume wa kitume.”

Mkiingia kwenye Basilika ya Pilar mtaona mchoro juu ya mawe ambapo anaonekana Yakobo akiwa na fimbo ya mhujaji, na pamoja naye wanaume wengine saba wanaomsindikiza.


Picha ya tokeo la Bikira Maria kwa mtume Yakobo.

Mapokeo yanasema kwamba Yakobo alikuwa amevunjika moyo, na kwamba Bikira alikuja (Mungu alifanya muujiza) na kumpa moyo wa kuendelea mbele: kitu cha ajabu kweli.

Bikira wa Pilar

Na kama ishara ya kuja kwake Zaragoza aliacha nguzo, nguzo ambayo kila mtu anaiheshimu (nyuma ya Bikira, inawezekana kuigusa, watu wanaigusa Nguzo hii; aliacha ukumbusho).

Kwenye uwanja huu, ukingoni mwa Mto Ebro, Basilika hii imejengwa, kwa heshima ya Bikira wa Pilar, ambaye sikukuu yake ni Oktoba 12, siku ya ugunduzi  wa Amerika.

Daraja na Katedrali-Basilika Bikira Maria wa Nguzo (“Virgen del Pilar” kwa kihispania)

Basilika hii inawasilisha yale yanayosema mapokeo ya mdomo, jinsi gani tangu uinjilishaji wa kwanza, baada ya ufufuko wa Yesu Kristo na Kupaa kwake mbinguni, Bikira Maria amewasindikiza mitume katikati ya matatizo yao, akiwasaidia wasife moyo hata kama wangeshindwa, kwa sababu kuinjilisha kunamaanisha kushindwa. Mtu, kibinadamu, mara nyingi hukata tamaa, anavunjika moyo, na Bikira Maria huja kumsaidia.

Kwa sababu hii – na nasema hivi kama utangulizi wa jumla- ni ajabu kuwa hapa ingawa kuna joto, hata kama hatuna raha, ishara na alama ya maana ya kuinjilisha: siku moja hatujui wapi kulala; siku nyingine kufunga; siku nyingine unakataliwa parokiani, ama kuna eneo lisilokukaribisha,…

Ni maisha ya mtume. Mungu alikuwa amechagua mahali hapa, ambapo Bikira alikutana na Yakobo na wasafiri wenzake, mitume, wakati tayari walikuwa wakipanga kuondoka wakishindwa. Na amewatia moyo ili kuinjilisha Hispania. Ni ishara ya Bwana kwa ajili yetu ya ajabu kweli.

Bikira wa Pilar

Maana yake ni kwamba kwa kazi hii, kazi hii ya uinjilishaji wa milenia ya tatu, ya vizazi vipya, tutakutana na magumu mengi, dhuluma nyingi, matatizo mengi, lakini hapa, Bikira Maria katika mahali hapa anatuambia kwamba atatusaidia. Hayo yawe kama mnara, kama Nguzo katika maisha yako ya kitume.

Mahali hapa huwakilisha kushindwa, ugumu, makwazo, matatizo ambayo kila mtume hukutana nayo. Kwa nini Bwana ametukusanya hapa? Kwa sababu katika mahali hapa, Bikira Maria amesaidia na kutegemeza washirika wake.

Bikira wa Pilar ambaye anaheshimiwa nchini Hispania ana picha ndogo. Bikira anapenda kuwa mdogo, mnyenyekevu, aliyefichwa. Kwa sababu hii, wakati mandamano yatakapoingia tutaimba “Maria, mdogo Maria.”


Carmen Hernández

Maneno ya Carmen kwenye Mkutano wa Miito:

Nina furaha sana kwamba tuko hapa, ukingoni mwa Mto Ebro, ambapo kwangu pia ni ukumbusho wa uwepo wa Bikira Maria katika historia yangu.

Nilizaliwa karibu sana na hapa, na nimekunywa maji kutoka mto huu kwa miaka 16, wakati bado hakukuwa na maji ya madini. Na ninafurahi sana, kwa sababu bibi yangu – eneo hili lote linamheshimu sana Bikira huyu – alikuwa na saa ambayo daima iliimba “Bikira Maria alikuja katika mwili wake mwenyewe Zaragoza.”

Kwa maneno mengine, kabla ya kufa, Bikira Maria alisindikiza uinjilishaji, yeye. Na mbele ya magumu ya mtume Yakobo, hapa pamoja na wahispania – na kutoka nchi hii, ambapo watu ni wakaidi sana, watu wa Aragon ni washupavu sana – na kwa vile mtume Santiago alikuwa amevunjika moyo alipoona haya yote, mapokeo yanasema kwamba Bikira Maria hapa katika mwili mwenyewe, huku Zaragoza (bado alikuwa hajapalizwa mbinguni, wala kufa, wala chochote …), yaani, Bikira daima alisindikiza uinjilishaji wa mitume, tangu kifo cha Yesu Kristo. . Nina furaha sana, kwa sababu hapa Bikira atakuwa Nguzo kwako, mnara wa kweli katika maisha yetu.


Zaragoza

Mwishoni mwa Siku ya IV ya Vijana Duniani ya 1989 ulioitishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II huko Santiago de Compostela, Kiko na Carmen waliwakusanya vijana wa Njia kwenye Mkutano wa Miito huko Zaragoza mnamo Agosti 21, mkesha wa Maria Mtakatifu Malkia:

Vijana 20,000 walikusanyika katika Uwanja wa Pilar.

Kiko na Carmen kwenye mkutano wa miito huko Zaragoza 1989

Ili kutembelea Zaragoza, tuma barua pepe kwa:
Humo utaeleza siku na saa unayotamani na idadi ya wahiji.

Pakua kipeperushi (kwa kihispania)
Share: