Tangazo kutoka kwa Njia ya Neokatekumenato kutokana na kufariki kwake Papa Fransisko

21 Aprili 2025 Kiko, Padre Mario na Ascensión, wajibikaji duniani wa Njia ya Neokatekumenato, pamoja na Ndugu wote wa Njia wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu, Papa wetu Fransisko. Jana, katika ujumbe wake wa Pasaka Urbi et Orbi (maana yake “kwa mji (Roma) na kwa dunia nzima”), ametupatia ushuhuda wake wa mwisho wa imani: “Ndugu wapendwa: Katika Pasaka ya Bwana, kifo na uzima zimekabiliana katika pambano la ajabu,

App ya kitabu cha nyimbo «AMEFUFUKA» inapatikana sasa.

Tunayo furaha ya kutangaza kwamba aplikesheni rasmi ya Kitabu cha Nyimbo “AMEFUFUKA” sasa inapatikana kwa usakinishaji, katika lugha kadhaa, kwenye vifaa vya Android na iOS (Apple): Aplikesheni hii mpya inatoa namna rahisi na inayoweza kufikiwa ili kutafuta na kupata nyimbo zote kutoka kwa “AMEFUFUKA”, iliyo bora kwa waimbaji wa jumuiya na ndugu wengine ambao wangependa kuwa na nyimbo kamili karibu. Ni hapa pekee, ambapo mtaweza kupata matoleo rasmi ya nyimbo zote,

Moyo usiogawanyika, utume na ubikira katika Carmen Hernández

Kimechapishwa kitabu kipya kuhusu Carmen, mwanzilishi mwenza pamoja na Kiko  Argüello wa Njia ya Neokatekumenato, na kinastahili kuzingatiwa nasi. Tunsaema kuhusu kitabu kinachoitwa Corazón Indiviso, misión y virginidad en Carmen Hernández, (“Moyo Usiogawanyika, utume na ubikira katika Carmen Hernández”) iliyoandikwa na Josefina Ramón, mshiriki katika Njia wa Neokatekumenato, na ambaye, kwa kufuata nyayo za Carmen, ni pia mseja na mmisionari msafiri, na kwa kuwa alilishwa na maisha na utajiri wa