Kumgundua Charles de Foucauld katika Mapango ya Farlete
“Huko nilikaa siku tatu katika pango, pango la Mtakatifu Kaprasi, peke yangu, bila kula, nikimsoma Charles de Foucauld, ambaye alinipa tia namna ya kuishi katika uwepo wa Bwana.”
Kiko, katika Kuishi Pamoja ya Mwanzo wa Mwaka 2016-2017
Kabla ya kuanza safari kupitia Ulaya, na kwa kuitayarisha, Padre Aguilar alitaka kumpe-leka Kiko kwenye jangwa la Los Monegros, huko Farlete (mkoa wa Zaragoza), ambapo Ndugu Wadogo wa Charles de Foucauld walikuwepo. Hapa Kiko alipata kumfahamu Padre R. Voillaume, mwanzilishi wa Ndugu Wadogo, na kusoma maisha ya Charles de Foucauld, akiwa ame-vutiwa sana, hasa, na ugunduzi wa maisha yaliyofichika ya Yesu na ya Familia ya Nazareti.
Taasisi ya Juan March ilimtunuku mwanateolojia Mdominiko ruzuku kwa ajili ya kutafuta mahusiano kati ya sanaa ya kiprotestanti na sanaa ya kikatoliki, kwa kulenga Mtaguso wa Vatikano II. Nilialikwa niende naye […] Kabla ya kuanza safari hiyo, kwa vile mwanateolojia Mdominiko aliwajua Ndugu Wadogo wa Foucauld, aliniambia hivi: “Kiko, kabla ya kuanza safari hii, itakayochosha sana, kwa sababu inatubidi kutembelea nchi nyingi, ningependa kukualika uende katika jangwa la Los Monegros, huko Farlete, katika jimbo la Zaragoza” […]. Tulikwenda na kukaa kwa wiki moja katika mafungo, tukijiandaa kwa safari. Katika jangwa hilo, ambalo ni zuri sana na lina pia mapango kadhaa […] Nakumbuka kwamba nilikuwa huko siku tatu katika “Pango la Mtakatifu Kaprasi”, nikisaidia. Huko nilifahamu maisha ya Charles de Foucauld. Nilizungumza na Padre Voillaume na nilishangaa sana na maisha ya siri ya Familia ya Nazareti na upendo mkuu wa Charles de Foucauld kwa uwepo halisi wa Kristo. Huko Tamanrasset (Algeria) alikaa kwa masaa peke yake mbele ya Sakramenti Takatifu.
K. Argüello, Kerigma. Katika vibanda pamoja na maskini, Madrid: 2012, uk. 29-30
Wakati Kiko alienda kwenye vibanda vya Palomeras Altas, alienda akifuata nyayo za Charles de Foucauld katika maisha ya siri ya Kristo, bila mpango wowote wa msaada wa kijamii. Kiko anasimulia hivi: “Sikwenda huko kuwafundisha watu hao kusoma na kuandika, wala kusaidia jamii. au hata kuhubiri Injili. Nilikwenda huko ili kujiweka kando ya Yesu Kristo. Charles De Foucauld alikuwa amenipatia njia ya kuishi miongoni mwa maskini kama mtu maskini, kimya kimya. Mtu huyu alijua jinsi ya kuishi katika uwepo wa kimya wa ushahidi kati ya maskini. Lengo lake lilikuwa maisha ya siri ambayo Yesu aliishi kwa miaka thelathini huko Nazareti, bila kusema chochote, kati ya wanadamu. Hii ilikuwa tasaufi ya Charles de Foucauld: kuishi kwa ukimya kati ya maskini. Foucauld alinipa kanuni ya kuifikia shabaha yangu ya kimonaki: kuishi kama maskini kati ya maskini, kushiriki nyumba yao, kazi yao na maisha yao, bila kuomba mtu yeyote chochote wala kufanya chochote maalum. Sikuwahi kufikiria kuanzisha shule au zahanati au kitu kama hicho. Nilitaka tu kuwa miongoni mwao nikishiriki uhalisia wao.”
Vibanda huko Palomeras Altas, Madrid, mwaka 1964
Ndugu Charles alika masaa mengi katika sala ya kitaamuli mbele ya Sakramenti na alikuwa na ndoto:
“Naamini ni wajibu wangu kupata eneo linalowezekana la Mlima wa Heri, ili kuhakikis-ha umiliki wake kwa Kanisa, na kisha kulikabidhi kwa Wafransisko, pamoja na kujitahidi kujenga altare ambapo, daima, misa itaadhimishwa kila siku na ambapo Bwana Wetu awepo katika Sakramenti…”
Ndoto ya Mtakatifu Charles de Foucauld ilitimia mnamo 2008, ampabo katika Senta ya Kimataifa ya Domus Galilaeae, iliyopo kwenye Mlima wa Heri (Korazim – Galilaya), kanisa dogo lilizinduliwa, lenye uwepo wa kudumu wa Ekaristi Takatifu, mchana na usiku. kwa ajili ya kuabudu daima Sakramenti Takatifu mahali hapa. Ni mahali ambapo panaakisiwa katika Ziwa la Galilaya na ambapo palirembeshwa na mahubiri ya Hotuba ya Mlimani ya Bwana, kama vile na ndoto ya Charles de Foucauld na pia kwa usanifu wa pekee, kazi nzuri ajabu ya Kiko Argüello.