Mt. Yohane Paulo II

Mt. Yohane Paulo II

Wasifu

Mt. Yohane Paulo II

Karol Józef Wojtyła, alizaliwa huko Wadowice (Kraków) mnamo Mei 18, 1920.

Mnamo Novemba 1, 1946, alipadrishwa huko Krakow. Mnamo 1948 alipata Udaktari katika Teolojia.

Mwaka 1958 aliteuliwa kuwa Askofu, mwaka 1964 akateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Krakow na Paulo VI, aliyemfanya kuwa Kardinali mwaka 1967.

Tarehe 16 Oktoba 1978, alichaguliwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki akichukua jina la Yohane Paulo II.

Alishiriki katika Mtaguso wa Vatikano II kwa mchango muhimu katika kufafanua katiba Gaudium et spes.

Alifanya idadi kubwa ya safari za kitume ndani na nje ya Italia. Mnamo 1985, alianzisha Siku za Vijana Duniani (SViD). Mnamo 1994, alianzisha mikutano ya familia duniani .

Upapa wake umekuwa kati ya zile ndefu zaidi katika historia ya Kanisa.

Yohane Paulo II alifariki tarehe 2 Aprili 2005. Alitangazwa kuwa Mwenye Heri tarehe 1 Mei 2011 na Papa Benedikto XVI na kutawazwa kuwa Mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014 na Papa Fransisko.


Hati