Ufafanuzi wa Njia ya Neokatekumenato
Njia ya Neokatekumenato ni safari ya malezi ya kikatoliki inayotekelezwa katika majimbo kupitia huduma za bure (taz. Kifungu cha 4 cha Statuta za Njia ya Neokatekumenato), iliyoidhinishwa na Kiti Kitakatifu. Mikusanyiko ya maadhimisho ya jumuiya hutumia nyenzo mbalimbali (nyimbo, ishara za kiliturujia na michoro), ambazo ni matunda ya ubunifu wa Kiko Argüello na Carmen Hernández, ambao, bila kutafuta faida, wamezifanya zipatikane bila gharama yoyote kwa ndugu wa jumuiya na parokia