Maaskofu na maaskofu wakuu mia mbili na hamsini kutoka mabara matano, wakisindikizwa na wamisionari wasafiri, mapadre na walei, pamoja na kikundi cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato katika majimbo yao (jumla ya ndugu zaidi ya 500), walialikwa na kikundi cha kimataifa cha wajibikaji wa Njia -Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero- katika mkutano huko Nchi Takatifu.

Mwaliko huo kwa Nchi Takatifu ulithibitishwa na barua kutoka kwa Mwadhama Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kanisa la kilatini huko Yerusalemu, ambaye hata hivyo hakuweza kuhudhuria kwa sababu ilimpasa kwenda kwenye mikutano ya makardinali na mazishi ya Baba Mtakatifu. Washiriki, waliofika katika Nchi Takatifu siku ya Jumatatu ya Pasaka, walishangazwa na kifo cha Papa Fransisko. Na habari hii ikawa sehemu ya kwanza ya ushirika kati yao wote: sala ajilia kwa roho ya Papa Fransisko na kwa ajili ya mkutano wa makardinali ambao ungefuati ili kumchagua Papa mpya.

Mkutano ulianza katika Domus Galilaeae (“Nyumba ya Galilaya”), kituo kilichopo kwenye Mlima wa Heri, ambapo maaskofu walipata fursa ya kuonjs siku za ushirika na sala, wakitembelea mahali patakatifu karibu na Bahari ya Galilaya: Korazini, Kapernaumu, Tabgha, pamoja na mahali ambapo Petro alipokabidhiwa upys nafasi yake ya kwanza kati ya Mitume, nk… huku wakipokea rehema kamili huko Nazareti.

Wakati wote wa mkutano huo, Kiko Argüello, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato pamoja na Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández, amewajulisha maaskofu baadhi ya vipengele vya uanzishwaji wa Kikristo ambao Njia hiyo inaleta katika majimbo, akifafanua baadhi ya misingi ya kikatekesi na kikerigma (tangazo la Habari Njema), ambayo inaunda safari hii ya imani.

Maaskofu walipata fursa ya kutafakari, katika vikundi kutokana na lugha waliyotumia, juu ya changamoto kubwa ambazo nyakati zetu zinaleta kwa Kanisa la leo, wakisisitizia hasa juu ya misukosuko yote katika familia, pamoja na matokeo yasiyoepukika kutokana na ukosefu wa watoto, upweke wa watu, kutelekezwa kwa wazee… Kwa sababu maaskofu walitoka katika mataifa mengi sana, mazungumzo hayo yalikuwa yenye kutajirisha sana kwa washiriki wote, wakishirikishana mateso ya makanisa yaliyo sasa matupu, kama vile yale yanayoteswa kwa kukosa uhuru au kwa ukatili wa siasa zenye msimamo mkali kupitiliza. Maaskofu walithamini sana jibu ambalo Njia ya Neocatekumenato inatoa kulingana na uzoefu wake wa miaka 60 wa uinjilishaji.

Mkutano uliendelea na hija ya siku mbili kwenda Yerusalemu. Makardinali na baadhi ya Maraisi wa Mabaraza ya Maaskofu, pamoja na baadhi ya Maaskofu kutoka Argentina, waliokuwa tayari katika Nchi Takatifu kwa ajili ya mkutano huo, walipaswa kurehea Roma kushiriki mazishi ya Baba Mtakatifu. Wengine wote waliweza kufuatilia liturjia ya mazishi kwa hisia kubwa kutoka kwenye skrini kubwa iliyokuwepo katika uwanda mpana wa Domus Betaniae (“Nyumba ya Betania”), kituo ambacho kinawapa mapadre na walei muda wa malezi na wa kuzamishwa katika maeneo matakatifu yanayotajwa katika Biblia.

Katika Taasisi ya Kipapa ya Notre Dame ya Jerusalem Center, mkutano ulifanyika pamoja na Askofu Mkuu Adolfo Tito Yllana, Balozi wa Papa nchini Israeli, kama vile pamoja na Meya wa Yerusalemu Moshe Lion. Walisisitiza jindi kurudi kwa mahujaji wa kikristo ni jambo la msingi na jinsi uwepo wa maaskofu wengi hivi, ambao wamehiji katika hali ya utulivu kabisa, unaweza kuchangia pakubwa katika kuwarejesha mahujaji wengine.

Balozi wa Kitume, pamoja na kukazia umuhimu wa Njia ya Neokatekumenato katika Kanisa, ameitakia Yerusalemu amani, kama chemchemi ya matumaini kwa dunia nzima. Meya wa Jerusalem, baada ya kutoa salamu zake nyofu kabisa za rambirambi kwa kuondokewa na Baba Mtakatifu Fransisko, aliwakaribisha waliohudhuria kwa moyo mkunjufu.

Mwishowe, Kiko Argüello alitoa maneno ya shukrani kwa maofisa mbalimbali, kwa Balozi wa Papa, pamoja na makasisi wengi walioshiriki katika mkutano huo, akimalizia kwa wimbo kutoka kwa nabii Isaya: “Nakuja kukusanya mataifa yote; watakuja waone utukufu wangu.” Unabii ambao ulitimizwa kwa kuona furaha ya maaskofu hawa wote waliotoka katika mabara matano.

Mkutano ulikamilishwa kwa kutembelea Chumba cha Karamu ya Mwisho—pengine umekuwa wakati wa kusisimua zaidi kwa maaskofu wengi—na ukahitimishwa kwa ziara ya maaskofu kwenye Kaburi Takatifu la Yesu na kisha kwenye Basilika ya Kuzaliwa kwa Bwana huko Bethlehemu, ambako walipokea tena rehema kamili. Tumeweza kuthibitisha katika wengi miongoni wa maaskofu walioshiriki hisia ya dhati ya shukrani kwa maang’amuzi ya pekee waliyoshiriki.


Kuona picha nyingine…

Njia ya Neokatekumenato
Kuishi Pamoja ya Maaskofu katika Domus Galilaeae 22-27 Aprili 2025

Share: