Leo asubuhi, tarehe 5 Juni 2025, saa tano asubuhi, katika Maktaba ya Ikulu ya Kitume, Baba Mtakatifu Leo XIV amepokea kwa mara ya kwanza kwa faragha Kikundi cha Kimataifa ya Njia ya Njia ya Neokatekumenato, Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi, na María Ascensión Romero.

Kiko alimsalimia Papa, akimwambia kwamba alikuwa na furaha sana kwamba Mungu ametupa Papa mmisionari, kwa sababu hii pia ndio utume wa Njia ya Neokatekumenato, katika nchi zisizomjua Kristo kama vile katika nchi ambazo zimemwacha.

Kiko alimzawadia nakala ya mchoro wa Bikira Maria wa Njia, ambao mchoro wake halisi uko katika Kanisa Kuu la Madrid, ambamo yameandikwa maneno yanayoeleza kwa kifupi utume wa Njia: “Inabidi kuunda jumuiya kama Familia Takatifu ya Nazareti, zinazoishi katika unyenyekevu, urahisi na sifa. Mwingine ni Kristo”. Pia alimzawadia Baba Mtakatifu nakala ya kitabu1 cha mwisho kuhusu Carmen, kiitwacho “Moyo usiogawanyika, utume na ubikira”, chenye nukuu zaidi ya 400 za Carmen kuhusu wanawake, kielelezo cha teolojia yake, zawadi ambayo Papa alipokea kwa shukrani.

Kiko pia alikumbusha kwamba ilikuwa sababu ya furaha kubwa kwamba uchaguzi wake ulifanyika Mei 8, Sikukuu ya Bikira Maria wa Pompeii, kwa sababu kumbukumbu hii, siku hii, ina umuhimu maalum kwa ajili ya Njia.

Papa alishangazwa na sadfa hii, na Kiko alimweleza jinsi mwaka 1968, baada tu ya kuwasili Italia pamoja na Carmen Hernández, alipelekwa Pompeii ili kuweka Njia ya Neokatekumenato chini ya ulinzi wa Bikiria Maria wa Pompeii. Tena, hivyo Kiko alisimulia, mnamo Mei 8 1974 ilikuwa kwa mara ya kwanza Papa, kipindi hicho Mtakatifu Paulo wa Sita, aliwapokea waanzilishi wa Njia pamoja na makatekista wasafiri wengine katika hadhira na kuwaambia maneno ya kinabii sana ambayo yamekuwa ya msaada mkubwa kwa Njia: “Tazameni matunda ya Mtaguso… Ninyi, kwa vile mlivyo, tayari mnafanya utume.” “Mnafanya yale ambayo Kanisa la kwanza lilifanya kabla ya ubatizo; ninyi mnafanya baadaye; kabla au baada, si muhimu; swala ni kwamba ninyi mnatazamia uhalisi, utimilifu, uwiano sawia, unyofu wa maisha ya Kikristo, na hili ni jambo linalotufariji sana.”

Katika mkutano huu uliojaa upendo wa mahusiano, Kikundi cha Kimataifa kiliweza kumjulisha Papa kuhusu shughuli nyingi za Njia zinazosongeshwa mbele ndani ya Kanisa, kupitia safari ya uanzishwaji wa kikristo unaotolewa kwa parokia na majimbo, kwa kutegemeza familia mbele ya changamoto za ulimwengu wa kisasa, zikiishi wito wao, zikiwa wazi kwa uhai kikamilifu, na kwa kuwapatia vijana wengi fursa ya kukutana na Yesu Kristo, Pekee ambaye anajibu sawasawa kwa mahitaji yao.

Papa Leo XIV pia alistaajabia idadi kubwa ya familia ambazo, kwa kumshukuru Bwana kwa maisha mapya waliyopata kwake, zimejitolea kusaidia utume wa Kanisa katika maeneo maskini na magumu zaidi ya dunia. Alishangazwa pia na uwepo wa Njia katika mataifa 138, idadi ya seminari za Redemptoris Mater zilizofunguliwa mpaka sasa katika majimbo zaidi ya mia katika mabara yote matano, pamoja na wanaseminari wengi wanaojiandaa kuwa mapadre wa kimisionari wa kijimbo.

Kikundi cha Kimataifa cha Njia pia ilipata fursa ya kumjulisha Papa kuhusu kazi ya uinjilishaji inayofanywa na wamisionari wasafiri wengi sana katika majimbo mbalimbali za dunia, katika nchi nyingi ambako pia yanatokea vile vile magumu yale yaliyo alama ya utume wa kimisionari.

Baba Mtakatifu aliwahimiza waendelee na huduma hiyo, yenye thamani kubwa hivyo kwa uhai wa Kanisa, na kwa baraka yake akaithibitisha Injili ya siku ile, kutoka Mtakatifu Yohane (Yn 17:20-26) ambayo inazungumzia upendo na umoja, njia inayompeleka mwanadamu wa leo kukutana na imani, neno linalopendwa sana na Baba Mtakatifu hivi kwamba ameliweka kama kauli mbiu katika ngao yake, ikisomwa In illo Uno, Unum, yaani “Katika yeye Mmoja (Kristo), (tunakuwa) Mmoja”, kauli ambayo imeonekana sana katika maang’amuzi ya Kiko na kutia alama yake katika uundaji wa Njia ya Neokatekumenato.



Share: