Roma, 22-26 Juni 2022
Njia ya Neokatekumenato Siku ya Kumi wa Familia Duniani huko Roma mwezi wa Juni 2022

Kuanzia tarehe 22 hadi 26 Juni, 2022, Mkutano wa Kumi wa Familia Duniani uliadhimishwa mjini Roma, ukiandaliwa na Idara kwa Walei, Familia na Uhai pamoja na Jimbo la Roma.

Wakiwakilisha Njia ya Neokatekumenato zilikuwepo familia kadhaa zilizotumwa na majimbo tofauti: Massimo na Patrizia Palloni, wenye watoto 12 (wasafiri, katika utume huko Uholanzi), Francesco na Sheila Gennarini, wenye watoto 9 (wasafiri, katika utume nchini Marekani), Dino na Roberta Furgione, wenye watoto 9 (wasafiri, katika utume nchini Afrika ya Kusini) na mpresbiteri Gianvito Sanfilippo (anayesimamia kipindi cha baada ya kipaimara katika Njia ya Neokatekumenato).

Asubuhi ya Ijumaa, Juni 24, mada mbalimbali zilijadiliwa. Maoni ya Massimo na Patrizia Palloni yalilenga “Upitishaji wa imani kwa vijana wa leo”: Massimo alielezea kwa ufupi maang’amuzi yake kama mwana, yeye alipokea imani kupitia wazazi wake katika Njia, na kwamba pamoja na mke wake, akiwa yeye pia mtoto wa wananeokatekumenato, wameipitisha kwa watoto wao 12. Haya ni madokezo mafupi ya Massimo na Patrizia:


Wadhama na Wahashamu, Wajumbe wa Mabaraza ya Maaskofu na wa Mikondo, ndugu wapendwa:

Tumeombwa kuzungumza juu ya mada ya “Upitishaji wa imani kwa vijana wa leo”, kutokana na maang’amuzi yetu binafsi. Tunawashukuru kwa nafasi hii mliyotupatia ya kumpa Mungu utukufu.

Sisi ni Massimo na Patrizia Palloni, kutoka jumuiya ya Neokatekumenato ya huko Roma na wamisionari wasafiri nchini Uholanzi kwa miaka kumi na minane. Wazazi wetu pia wako katika jumuiya na kupitia maang’amuzi yao wametupitishia imani. Kwa hiyo, tunaweza kuzungumza kuhusu maang’amuzi yetu kama watoto – ambao wazazi wao wamewapitishia imani – na pia kama wazazi wa watoto kumi na wawili, ambao wako hapa; wanawasalimu na pia wanawashukuru.

Katika uhusiano wetu na wazazi wetu, na leo pamoja na watoto wetu, tumeongozwa na Neno ambalo Mungu aliwapa watu wake alipotokea kwenye Mlima Sinai:

“Sikiliza, Israeli: Bwana ndiye Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na yabaki moyoni mwako maneno haya ninayokuamuru leo​​. Utayarudia kwa watoto wako, utawazungumzia juu yao uwapo nyumbani au safarini, ulalapo na uamkapo” (Kumb 6,4-7).

Tangu tulipokuwa wadogo, wazazi wetu waliadhimisha masifu nasi Jumapili asubuhi. Baada ya kuimba zaburi, somo kutoka Biblia lilitangazwa na tulisaidiwa kuona maisha yetu katika nuru ya Neno la Mungu. Pia tangu tukiwa wadogo sana Neno hili limeangazia mahusiano yetu na kaka zetu, dada zetu na wazazi, likituruhusu kupatana na kuzungumza juu ya mateso yetu. Baba yetu alituuliza: “Je! Neno hili linaangaziaje uhalisia wako wa leo?”; swali hili ni mwangwi wa lile swali la kwanza linalopatikana katika Biblia: “Adamu, uko wapi?” Kama Papa Fransisko alivyosema katika Amoris Laetitia: “Basi swali kuu sio mtoto yuko wapi kimwili, ama yuko na nani wakati huu, lakini yuko wapi katika maana ya kiutu”[1]. Neno la Mungu linakuwa kielelezo cha maisha yote ya mwanadamu, kila neno lililomo ndani yake linaangazia historia yetu: uumbaji, safina ya Nuhu, gharika kuu, mnara wa Babeli, Abrahamu, Kutoka, mithali ya Injili, nk. Neno hili pia limeangazia maisha yetu tangu tukiwa watoto; lilikuwa daraja la ajabu kati ya wazazi na watoto, kati ya vizazi tofauti. Kila mmoja wetu alikuwa na uwezekano wa kutoa maang’amuzi yake mwenyewe. Kupitia kukutana katika sala, Bwana alitusaidia kweli kweli kuelewa “tulikuwa wapi”, kuelewa mateso ya wengine na, mara nyingi sana, kupatana. Siku zote masifu zilifuatiwa na mlo wa pekee ili kuishi Jumapili kikamilifu.

Aidha, kila mwaka tuliingizwa katika familia kwa sherehe kuu zilizoandaliwa kwa uangalifu mkubwa, ambazo ziliashiria majira na ambazo tuliishi na parokia nzima: Krismasi, Epifania, Pentekoste, Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili… Baada ya komunyo ya kwanza, sisi tulishiriki kiaminifu katika Ekaristi katika jumuiya, ambamo tulipokea uangalifu wa pekee. Ekaristi hii, tuliyoishi parokiani baada ya jioni ya kwanza ya Jumapili, imetung’oa taratibu kutoka dhambi za Jumamosi usiku, ambazo zinawapeleka vijana kujitenga na Kristo. Katikati ya yote ulikuwa Mkesha wa Pasaka, ambao kwao tuliingizwa na kuusubiri kwa hamu. Hivyo, tuliingizwa hatua kwa hatua katika maisha ya imani ndani ya Kanisa, na tukiwa katika ujana, tuliingia -pamoja na vijana na watu wazima wengine- katika jumuiya ya parokia ili kuendeleza uingizwaji wa kikristo. Isitoshe, kila mara, tulishiriki katika hija na Siku za Vijana Duniani, ambapo tulisaidiwa kutafakari kwa kina wito wetu na kupokea neno la Baba Mtakatifu. Mikutano hii imekuza ndani yetu upendo kwa Papa na kwa Kanisa zima.

Gradualmente, a lo largo de los años, hemos gustado la maravilla de la vida cristiana. Nos ha sido transmitido que en el centro de la familia existen tres altares[2]: el primero es la mesa de la Santa Eucaristía, en el que Jesucristo ofrece el sacrificio de su vida y su resurrección por nuestra salvación; el segundo es el tálamo nupcial donde, al ofrecerse el uno al otro, se cumple el Sacramento del Matrimonio y se da el milagro del amor y de la nueva vida; el tercero es la mesa donde la familia se reúne para comer, bendiciendo al Señor por sus dones. Así, cada comida, se convierte en un encuentro en el que se discuten los temas y los problemas que se encuentran en la vida o en la escuela, donde todos participan y se vive la comunión.

Tulipooana tulikuwa vijana sana, mimi nilikuwa na miaka ishirini na minne na Patricia ishirini, na ingawa tulifunga ndoa tukiwa na nia njema ya kuunda familia ya kikristo, katika miaka ya kwanza ya ndoa tulijikuta mbele ya madhaifu yetu ambayo yalihatarisha muungano wetu. Katika hali hiyo ya ugumu, kilichotutegemeza ni jumuiya yetu iliyoundwa na watu wa kawaida ambao, kama sisi, wakiishi safari ya imani, walitusaidia kushinda misukomisuko yetu wakizungumza nasi katika ukweli na kutualika kutambua makosa yetu, kupitia uhusiano wetu na Sakramenti na Neno la Mungu lililoangazia uhalisia wetu wa dhambi.

Kwetu sisi huo ulikuwa mwanzo mpya, kama vile kwenye harusi ya Kana: ambapo baada ya kuishiwa na “divai” ya kushikwa na upendo mmoja kwa mwingine na kupendana kutokana na jitihada zetu, Yesu Kristo alitupatia bure divai mpya, yenye kulewesha, ya msamaha. Tumegundua kwamba kuwa wazi kwa uhai si sheria inayolemea bali ni ukombozi kutoka uchoyo, ukombozi ambao bila huo ndoa inayumba. Kwa mshangao mkubwa, Mungu amtejualia kumtarajia kwa hamu kila mtoto ambaye ametuzawadia. Bwana amekuwa mkuu kuliko dhambi zetu na, licha ya madhaifu na kutoweza kwetu, leo tuko hapa pamoja na watoto wetu kumi na wawili ambao kwetu ni uthibitisho usiopingika wa uaminifu wa Mungu.

Kupitisha imani kwa vijana wa leo: kazi muhimu sana ambayo leo inahusu Kanisa na kila mbatizwa. Tumezama katika jamii ambayo inaonekana kwamba Mungu ametoweka kutoka upeo. Uduniaisho kusonga mbele kwa kasi kubwa sana, kupoteza maana ya Mungu, majeraha ya utoaji mimba na ya euthanasia ni tishio la kila siku kwa imani ya kila mtu. Shambulio la shetani linataka kuharibu familia na vijana: janga la ponografia mtandaoni ambalo leo limefikia ulimwengu mzima, madawa ya kulevya, kuchanganyikiwa katika mtu kujua yeye ni nani, maono ya kinyosi ambayo hutenganisha mtu na mwili wake. Papa Fransisko amefafanua usambaaji wa itikadi ya jinsia kuwa ni vita: «Leo kuna vita vya dunia kwa ajili ya kuharibu ndoa […] lakini si kwa silaha, bali kwa mawazo», ni «ukoloni wa kiitikadi unaoharibu»[3].

Muda wa ubalehe na wa ujana labda ni ule mgumu zaidi katika malezi ya mtu: ni wakati ambapo mabadiliko makubwa ya kimwili, kiakili na ya kihisia hufanyika, ambapo eneo la mahusiano ya kijamii hupanuka (kuingia katika shule ya juu, kujitegemea na familia, urafiki mpya) na ni hasa katika kipindi hiki chororo, ambapo mahusiano na wazazi yanakuwa na migogoro zaidi, ambapo vijana wanapaswa kufanya maamuzi ya msingi ambayo yataathiri maisha yao yote. Mbele ya hali hizi, Roho Mtakatifu ameinua mang’amuzi mengine ya kuwasaidia vijana wa parokia: mang’amuzi ya baada ya kipaimara.

Leo, vijana wengi sana wanatokea familia zilizojeruhiwa. Asilimia inayoongezeka kila mara zaidi ya watoto wanaishi na mzazi mmoja tu, wengi kutokana na kutengana kwa wazazi, sehemu nyingine kutokana na hali za nje ya ndoa. Wakikabiliwa na kushindwa kwa zaidi ya asilimia 50 ya ndoa, bila tegemeo na msaada wa shule, vijana wengi wanajikuta bila msingi wowote thabiti na wanapotea. Katika maang’amuzi mapya ya baada ya kipaimara, ambao maparoko wengi duniani kote, katika ushirika na maaskofu wao, wameamua kuanzisha, vikundi vidogo vya vijana vinaundwa ambavyo vinakutana na familia yenye imani thabiti na pevu, yenye uwezo wa kutoa ushuhuda halisi wa huduma kwa vijana hawa. Vijana wanavutiwa na familia ya kikristo ambamo wanaona imani hai. Katika makundi hayo, vijana wanaanza kusoma Neno la Mungu, kutafakari juu ya amri kumi kama njia ya maisha, wanagundua upya Sakramenti ya Upatanisho na kukutana na maisha ya kikristo ya familia halisi.

Maang’amuzi haya yanatoa matunda ya kuvutia sana katika parokia nyingi: kipindi cha baada ya kipaimara, ambacho kwa kawaida kina sifa ya vijana wengi kuacha, sasa kupitia kwa huduma hii inakuwa baraka kutoka kwa Bwana, kwani asilimia ya vijana wanaoendelea kuhudhuria parokia baada ya kipaimara ni juu sana. Isitoshe, furaha ya vijana hawa inasambaa na inakuwa ushuhuda kwa wenzao shuleni, marafiki, wanaofahamiana nao, ambao nao wanaomba kuishi furaha hiyo kwa kujiunga na vikundi na, kwa njia hii, vijana wengi walio mbali wanalikaribia kanisa.

Walakini, si swala la kutafuta njia au kutumia mbinu. Hakuna anayeweza kutoa kile ambacho hajapokea. Katika ” udikteta wa ‘inategemea’” unaotuzunguka, pamoja na “sheria” zake mpya zinazopotosha dhamiri za vijana wengi, kuna “muziki” ambao moyo wao hautaacha kamwe kuusikiliza au kuutambua kama mlango wa heri, yaani, upendo. Kwa sababu hiyo, katika uchungaji wa vijana, ushuhuda wa familia una umuhimu wa kimsingi, familia ambazo, zikiwa zimepokea upendo wa bure wa Kristo na Kanisa, zinawapokea kwa upendo huo huo vijana hawa waliojeruhiwa na kuuwasilisha upendo huu kwao kama kitu kilicho hai na cha sasa.

Nguvu nzima ya mvuto wa Ukristo iko katika nguvu ya ushuhuda, kama Mtakatifu Paulo VI alivyothibitisha: «Mtu wa wakati huu anawasikiliza kwa radhi zaidi wale wanaotoa ushahidi kuliko wale wanaofundisha (…) au akiwasikiliza wale wanaofundisha, ni kwa sababu ni mashahidi»[4].

Si kwamba vijana hawajali hukusu imani; ikiwa hawajali, ni kwa sababu hawaioni, kwa sababu wanachukia ugoigoi, undumilakuwili. Ikiwa wanatangaziwa ukweli, ikiwa watatangaziwa kuwa wanaweza kutoka katika utumwa wa “Umimi” wao, kwamba wanaweza kujitoa kabisa, watatufuata. Ndiyo, ikiwa sisi tunatabiri haya kwa vijana watatufuata kwa maelfu!

Na kwa hivyo tunarudi kwa swali la asili: Vipi kupitisha imani kwa vijana wa leo?

Leo, Kanisa linapitia katika msukosuko mkubwa ambao unapitia katika mahudhurio hafifu Kanisani Jumapili, idadi ndogo ya ubatizo, ndoa na sakramenti, miito kupungua. Hakika, si swala la idadi, lakini hata hivyo, inaonekana kwamba kila kitu kinaporomoka kwa haraka sana. Tukikabiliwa na hali hii, tunaweza kushawishiwa kufikiri kwamba jibu ni kutafuta tu mpango au kanuni, labda unaotegemea mawaidha ya kimaadili.

Ili kupitisha imani kwa vijana, imani ya wazazi inahitajika. Tuko hapa, si kusema kwamba tuko bora au kwamba tumepata mbinu, lakini kwa sababu wazazi wetu wamegundua upya imani hai ambayo imewasaidia katika ndoa zao na ambayo wamepitisha kwetu, watoto wao. Na watoto wetu wako hapa kwa sababu hiyo hiyo.

Ili kugundua upya imani inahitajika njia ambayo inawezakukuza ndani ya kila mwumini nguvu yenye kuhuisha ya Ubatizo. Hicho ndicho ulichoelekeza Mtaguso wa Vatikano II katika katiba kuhusu Liturjia Sacrosanctum Concilium[5] ikiurejesha ukatekumeni kwa ajili ya watu wazima ambao hawajabatizwa. RCIA (Uingizwaji katika Ukristo wa Watu Wazima)[6] –hati ya utekelezaji wa uamuzi wa Mtaguso- iliongeza umuhimu wa uamuzi huo ikithibitisha kwamba ukatekumeni unaweza kutumika kwa Wakristo ambao tayari wamebatizwa lakini ambao hawajapokea uingizwaji unaohitajika kwa ubatizo. Uamuzi huu wa kihistoria upo pia katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki ambapo inaelezwa kwamba “kwa asili yake, Ubatizo wa watoto unahitaji ukatekumeni baada ya ubatizo. Sio tu juu ya hitaji la mafundisho baada ya Ubatizo, bali juu ya unaohitajika wa neema ya ubatizo katika ukuaji wa mtu»[7].

Mtakatifu Paulo VI alitambua mwaka 1974 umuhimu wa kimsingi wa ukatekumeni baada ya ubatizo: «Kuishi na kuendeleza mwamko huu kunaangaliwa nanyi kama aina ya ukatekumeni baada ya ubatizo, ambao utaweza kuupyaisha katika jumuiya za kikristo za leo matunda yale ya upevu na ya kina ambayo katika Kanisa la mwanzo yalifanywa katika kipindi cha maandalizi ya Ubatizo. Ninyi mnaufanya baadaye: kabla au baada, ningesema, si muhimu. Swala ni kwamba ninyi mnatazamia uhalisi, utimilifu, uwiano sawia, unyofu wa maisha ya Kikristo Na hii ina stahili kubwa sana, narudia, ambayo inatufariji sana»[8].

Mbele ya msukosuko wa kutisha wa familia na wa vijana, inahitajika kugundua upya, kwa njia ya uingizwaji wa kikristo, msimamo mzizi wa Injili, kama ilivyotokea kwa Wakristo wa kwanza katikati ya ulimwengu wa kipagani.

Asanteni!


[1] Fransisko, Amoris Laetitia, 261.

[2] taz. Fransisko, Amoris Laetitia, 318.

[3] Fransisko, Hotuba ya Baba Mtakatifu wakati wa mkutano na mapadre na watawa, huko Tbilisi (Georgia), Oktoba 1, 2016.

[4] Paulo VI, Evangelii Nuntiandi, 41.

[5] Kama ilivyoelezwa na Mtaguso wa Pili wa Vatikani katika Sacrosanctum Concilium 64: «Uwekwe tena ukatekumeni kwa watu wazima, uliogawanywa katika hatua nyingi, wa kutekeleza kadiri ya mwongozo wa Mkuu mahalia. Hivyo, muda wa ukatekumeni, uliowekwa kwa ajili ya mafundisho yafaayo, uweze kutakatifuzwa kwa njia ya ibada takatifu zitakazoadhimishwa kwa nyakati mbalimbali». ». Hili pia lilithibitishwa baadaye na Ordo Initiationis Christianae Adultorum (OICA) ya mwaka wa 1972.

[6] RCIA (Uingizwaji katika Ukristo wa Watu Wazima), kwa Kilatini: OICA (Ordo Initiationis Christianae Adultorum). RICA, Sura ya IV.

[7] KKK (Katekisimu ya Kanisa Katoliki), no. 1231.

[8] Paul VI akielekeza neno kwa Jumuiya za Neokatekumenato, Hadhira, Mei 8, 1974.

Share: