Njia ya Neokatekumenato - SViD Ujerumani 2005 - Kiko Argüello
Kiko Argüello katika Mkutano wa Miito wakati wa Siku ya Vijana Duniani huko Cologne, Ujerumani mwaka 2005.

Ndugu wapendwa,

Kutoka Ureno tunawapatia taarifa kuhusu Siku ya Vijana Duniani (SViD) ijayo, huko Lisbon 2023.

Tarehe rasmi za siku hizo ni kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023. Mkesha na Baba Mtakatifu utakuwa Jumamosi tarehe 5 na Ekaristi ya mwisho Jumapili tarehe 6.

Tovuti rasmi (kwa kiingereza) ya SViD ni:

Kusajili kwa Mkutano huo, kwa zake mbalimbali, kutafunguliwa mwishoni mwa Oktoba.

Ni muhimu sana usajili rasmi, kwa sababu kadiri ya walivyotuambia, ni hivyo tu mabasi maalum yatatambua namna kuzunguka kwenye maeneo mbalimbali ya kupaki.

Mkutano wa Miito na Kiko, Mario na María Ascensión umepangwa kufanyika Jumatatu, Agosti 7. Baadaye tutatoa taarifa zaidi.

Senta ya Neokatekumenato ya Lisbon itaunda ukurasa wa tovuti ili kuwasaidia ndugu katika masuala ya maeneo kiini ya kutembelea, ratiba ya mzunguko, maeneo ya kufanya utume na hatimaye mahali fulani pa kuadhimishia.

Mtahitaji pia kujisajili katika tovuti yetu ili kuweza kuratibisha mkutano wa wito, namba ya washiriki, maaskofu, nk.

Tovuti ya hija kwa ajili ya ndugu wa Njia (kwa kiingereza) ni:

Yote yanayohusu malazi katika parokia, kumbi za michezo na mazoezi, nyumba za kitawa, nk., yatapangwa na kikundi rasmi kinachoandaa Mkutano; kwa vikundi ambavyo mtahitaji malazi, itawabidi kuomba kwa kujisajili rasmi kwenye taasisi inayoongoza SViD.

Linapokuja suala la hoteli, mnahitaji kupanga na wakala wa usafiri.

Tunamkabidhi Bikira Maria wa Fatima, atusaidie kufanya Mapenzi ya Mungu na kutusindikiza katika Siku hii ya Vijana Duniani na aamshe miito kati ya vijana wetu.

Mtuombee. Amani na hija njema.

Kikundi cha makatekista wasafiri wa Ureno, Pd. Angel Bello, Fernando na Ana, Davide.

Share: