Tamasha katika Kathedrali ya Cordoba, Hispania

Mateso ya wasio na hatia na Masiya, 19 Oktoba 2025 Orkestra na Kwaya ya Kisimfonia ya Njia ya Neokatekumenato ilitumbuiza huko Cordoba (Hispania), katika mazingira ya kuvutia ya Kathedrali yake, inayotambulika kwa muundo wake kama Msikiti, mbele ya kanisa lililojaa waamini na makasisi kadhaa. Miongoni mwao, waliohudhuria ni Askofu wao Mkuu, Monsinyori Jesús Fernández, pamoja na Askofu Mstaafu wa jimbo hilohilo, Monsinyori Demetrio Fernandez, na Askofu Mstaafu wa Jimbo la

Vijana 120,000 kutoka Njia ya Neokatekumenato huko Roma kwa ajili ya Jubilei na Papa na mkutano wa miito.

Kama hitimisho la Jubilei ya Vijana, iliyotakwa na Baba Mtakatifu Fransisko na kuadhimishwa na Baba Mtakatifu Leo XIV, ili kurejesha matumaini kwa dunia ya leo, vijana 120,000 kutoka jumuiya za Njia ya Neokatekumenato kutoka nchi 109 katika mabara matano wamekusanyika alasiri ya leo, tarehe 4 Agosti 2025, mahali pale pale pa mkutano na Papa, pamoja na Kikundi cha Kimataifa cha Kiko Argüello, María Ascensión na Padre Mario. Katika jukwaa kuu,

Papa Leo XIV ampokea Kiko Argüello, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato

Leo asubuhi, tarehe 5 Juni 2025, saa tano asubuhi, katika Maktaba ya Ikulu ya Kitume, Baba Mtakatifu Leo XIV amepokea kwa mara ya kwanza kwa faragha Kikundi cha Kimataifa ya Njia ya Njia ya Neokatekumenato, Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi, na María Ascensión Romero. Kiko alimsalimia Papa, akimwambia kwamba alikuwa na furaha sana kwamba Mungu ametupa Papa mmisionari, kwa sababu hii pia ndio utume wa Njia ya Neokatekumenato, katika nchi

Kazi za Kisimfonia ya Kiko Argüello: Njia ya Uzuri kwa ajili ya Uinjilishaji

Tafsiri yetu ya makala iliyochapishwa kwa idhini ya Vatican News Kutokana na hafla ya Jubilei ya Familia, simfonía zote mbili za mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, zilipigwa pamoja kwa mara ya kwanza jioni ya Juni 1, 2025, kwenye “Auditorio Parco della Musica” (“Ukumbi wa Bustani ya Muziki”)huko Roma: Monsinyori Fisichella asema: simfonia ya aina hii imetufundisha kuwa sisi si watazamaji bali washiriki. Débora Donnini – Mji wa Vatikano  Ni muziki

Onyesho la kimuziki kwa ajili ya Jubilei ya Familia

Kazi ya Kisimfonia ya Kiko Argüello pamoja na Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato, ikiwa imeongozwa na Tomáš Hanus Jubilei 2025 Jumapili, Juni 1, 2025, saa moja jioni, katika Ukumbi wa “Parco della Música Ennio Morricone”, kwenye Ukumbi wa Santa Cecilia, Kiko Argüello awasilisha Kazi yake ya Kisimfonia. Onyesho juu kwa ajili ya Jubilei ya Familia, ambapo Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato, inayoendeshwa na Tomáš Hanus, mkurugenzi wa Orkestra ya Kisimfonia

Uchaguzi wa Papa Leo XIV

Njia ya Neokatekumenato imepokea habari za kuchaguliwa kwa Kardinali Robert Prevost kuwa Khalifa wa Petro kwa furaha kubwa. Maneno yake ya kwanza yametujaza furaha, akimweka Kristo Mfufuka kama kiini cha yote, ambaye anatupatia amani yake, pamoja na uinjilishaji unaozaliwa kutoka katika moyo wa kimisionari. Kumekuwa na mwangwi wa pekee katika mioyo ya ndugu wote wa Njia—na hasa ule wa kwangu— kutokana na kwamba uchaguzi huu ulifanyika siku ya Bikira Maria

Maaskofu katika Nchi Takatifu wakialikwa na Njia ya Neokatekumenato

Maaskofu na maaskofu wakuu mia mbili na hamsini kutoka mabara matano, wakisindikizwa na wamisionari wasafiri, mapadre na walei, pamoja na kikundi cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato katika majimbo yao (jumla ya ndugu zaidi ya 500), walialikwa na kikundi cha kimataifa cha wajibikaji wa Njia -Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero- katika mkutano huko Nchi Takatifu. Mwaliko huo kwa Nchi Takatifu ulithibitishwa na barua kutoka kwa Mwadhama Kardinali