Kazi za Kisimfonia ya Kiko Argüello: Njia ya Uzuri kwa ajili ya Uinjilishaji

Tafsiri yetu ya makala iliyochapishwa kwa idhini ya Vatican News Kutokana na hafla ya Jubilei ya Familia, simfonía zote mbili za mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, zilipigwa pamoja kwa mara ya kwanza jioni ya Juni 1, 2025, kwenye “Auditorio Parco della Musica” (“Ukumbi wa Bustani ya Muziki”)huko Roma: Monsinyori Fisichella asema: simfonia ya aina hii imetufundisha kuwa sisi si watazamaji bali washiriki. Débora Donnini – Mji wa Vatikano  Ni muziki

Uchaguzi wa Papa Leo XIV

Njia ya Neokatekumenato imepokea habari za kuchaguliwa kwa Kardinali Robert Prevost kuwa Khalifa wa Petro kwa furaha kubwa. Maneno yake ya kwanza yametujaza furaha, akimweka Kristo Mfufuka kama kiini cha yote, ambaye anatupatia amani yake, pamoja na uinjilishaji unaozaliwa kutoka katika moyo wa kimisionari. Kumekuwa na mwangwi wa pekee katika mioyo ya ndugu wote wa Njia—na hasa ule wa kwangu— kutokana na kwamba uchaguzi huu ulifanyika siku ya Bikira Maria

Maaskofu katika Nchi Takatifu wakialikwa na Njia ya Neokatekumenato

Maaskofu na maaskofu wakuu mia mbili na hamsini kutoka mabara matano, wakisindikizwa na wamisionari wasafiri, mapadre na walei, pamoja na kikundi cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato katika majimbo yao (jumla ya ndugu zaidi ya 500), walialikwa na kikundi cha kimataifa cha wajibikaji wa Njia -Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero- katika mkutano huko Nchi Takatifu. Mwaliko huo kwa Nchi Takatifu ulithibitishwa na barua kutoka kwa Mwadhama Kardinali

Tangazo kutoka kwa Njia ya Neokatekumenato kutokana na kufariki kwake Papa Fransisko

21 Aprili 2025 Kiko, Padre Mario na Ascensión, wajibikaji duniani wa Njia ya Neokatekumenato, pamoja na Ndugu wote wa Njia wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu, Papa wetu Fransisko. Jana, katika ujumbe wake wa Pasaka Urbi et Orbi (maana yake “kwa mji (Roma) na kwa dunia nzima”), ametupatia ushuhuda wake wa mwisho wa imani: “Ndugu wapendwa: Katika Pasaka ya Bwana, kifo na uzima zimekabiliana katika pambano la ajabu,

Fuentes de Carbonero el Mayor (Segovia – Hispania)

«WAKATI MAWE YANAONGEA TENA» Oktoba 12 iliyopita (2022), sikukuu ya Bikira wa Pilar (Bikira wa Nguzo)- siku ambayo Hispania inaadhimisha kwa taadhima, kutokea kwake Bikira Mama wa Mungu kwa mtume Santiago na wenzake katika mwaka wa 40 BK kwenye nguzo ya marumaru kwenye ukingo wa mto Ebro, ili kuwatia moyo katika kuendelea na uinjilishaji – huko Fuentes de Carbonero el Mayor, kijiji kidogo karibu na Segovia kilichotelekezwa na watu tangu

Maoni mubashara katika hafla ya ufunguzi wa mchakato ya Kutangazwa kuwa Mwenye Heri kwa Carmen Hernández

Maoni ya Kiko Argüello Jioni njema kwenu nyote, Namsalimu Mha. Carlos Osoro, Kardinali-Askofu Mkuu wa Madrid. Mwadhama Kardinali Antonio Maria Rouco, Askofu Mkuu Mstaafu wa Madrid. Kardinali Paolo Romeo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Palermo. Maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi waliopo hapa. Mama Mkuu wa Wamisionari wa Kristo Yesu na washauri wake. Ni furaha gani unayotupatia uwepo wenu katika hafla hii, madada! Mkuu wa Chuo, Pd. Daniel Sada, Wakuu wa