Hija Fuentes de Carbonero el Mayor (Segovia – Hispania)

Kanisa la Fuentes de Carbonero Mahali pa kuhiji na kuadhimisha, ushuhuda wa historia ambayo Mungu hufanya pamoja nasi. «Nilishangaa sana kwamba wakati nyumba zote katika kijiji hicho ziliharibika, kitu pekee kilichobaki kikisimama katika kijiji hicho kilichotelekezwa kilikuwa kanisa, na kanisa ambalo limejaa maskini.Hapa tulisherehekea Mkesha wa Pasaka na ndugu wa vibandani na wale wa jumuiya ya kwanza ya Madrid. Hatukuwa na umeme; Tulijiangazia na nuru ya mshumaa mkubwa wa zamani

Maoni mubashara katika hafla ya ufunguzi wa mchakato ya Kutangazwa kuwa Mwenye Heri kwa Carmen Hernández

Maoni ya Kiko Argüello Jioni njema kwenu nyote, Namsalimu Mha. Carlos Osoro, Kardinali-Askofu Mkuu wa Madrid. Mwadhama Kardinali Antonio Maria Rouco, Askofu Mkuu Mstaafu wa Madrid. Kardinali Paolo Romeo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Palermo. Maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi waliopo hapa. Mama Mkuu wa Wamisionari wa Kristo Yesu na washauri wake. Ni furaha gani unayotupatia uwepo wenu katika hafla hii, madada! Mkuu wa Chuo, Pd. Daniel Sada, Wakuu wa

Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri kwa Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández

“Yesu wangu, nipeleke kwenye utakatifu wako”; “Wewe unaniongoza kwenye utakatifu” (“Kitabu cha kumbukumbu 1979-1981”, na. 85; na.199) Tarehe Desemba 4, 2022, “Tukio” lenye nguvu na maana maalum kwa Kanisa zima lilitukia huko Madrid: ufunguzi wa hatua ya kijimbo ya Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu kwa Carmen Hernández Barrera, mwanzilishi mwenza, pamoja na Kiko Argüello, wa njia hiyo ya uanzishwaji wa kikristo inayoitwa Njia ya Neokatekumenato. Ufunguzi wa mchakato Katika

Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu wa Carmen Hernández

Mubashara Kutoka Madrid (Hispania), jumapili tarehe 4 Desemba, 2022,  saa 2 usiku, East Africa Time (GMT +03:00)  Jimbo Kuu la Madrid Kituo cha michezo cha Chuo Kikuu cha Francisco Vitoria. Anaongoza ibada Kard. Carlos Osoro, Askofu Mkuu wa Madrid. Waanzilishi wa Mchakato: Kiko Argüello, P. Mario Pezzi, Ascensión Romero, Taasisi za “Familia ya Nazareti” za Roma na Madrid. Mwombaji: Carlos Metola.

Siku ya Vijana Duniani – SViD Lisbon 2023

Ndugu wapendwa, Kutoka Ureno tunawapatia taarifa kuhusu Siku ya Vijana Duniani (SViD) ijayo, huko Lisbon 2023. Tarehe rasmi za siku hizo ni kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023. Mkesha na Baba Mtakatifu utakuwa Jumamosi tarehe 5 na Ekaristi ya mwisho Jumapili tarehe 6. Tovuti rasmi (kwa kiingereza) ya SViD ni: Kusajili kwa Mkutano huo, kwa zake mbalimbali, kutafunguliwa mwishoni mwa Oktoba. Ni muhimu sana usajili rasmi, kwa sababu kadiri

Ushuhuda wa familia ya Njia ya Neokatekumenato katika Mkutano wa Kumi wa Familia Duniani.

Roma, 22-26 Juni 2022 Kuanzia tarehe 22 hadi 26 Juni, 2022, Mkutano wa Kumi wa Familia Duniani uliadhimishwa mjini Roma, ukiandaliwa na Idara kwa Walei, Familia na Uhai pamoja na Jimbo la Roma. Wakiwakilisha Njia ya Neokatekumenato zilikuwepo familia kadhaa zilizotumwa na majimbo tofauti: Massimo na Patrizia Palloni, wenye watoto 12 (wasafiri, katika utume huko Uholanzi), Francesco na Sheila Gennarini, wenye watoto 9 (wasafiri, katika utume nchini Marekani), Dino na

Papa kwa familia za Njia ya Neokatekumenato zilizotumwa katika utume

Kiko Argüello Baba Mpendwa: Asante kwa uwepo wako, asante kwa kukubali kutuma familia hizi katika utume. Tunawasalimu Kardinali Kevin Farrell, Maaskofu wakuu na Maaskofu waliopo, na pia washiriki kutoka Idara ya Walei, Familia na Uhai, ambao wamekubali kushiriki tukio hili pamoja nasi. Baba Mtakatifu, kabla hatujaanza, tunataka kukushirikisha habari ambayo tunajua itakufurahisha: Jimbo kuu la Madrid limetufahamisha kwamba mchakato wa kutangazwa kuwa mwenye heri na wa kuwa mtakatifu wa Carmen