Maelfu ya vijana watashiriki katika mkutano wa miito wa Njia ya Neokatekumenato huko Lisbon ndani ya mfumo wa SViD (Siku ya Vijana Duniani).

Jumatatu ijayo, Agosti 7, watakutana kutoka mabara matano pamoja na makardinali na maaskofu mbalimbali Njia ya Neokatekumenato, kama ilivyo desturi katika Siku za Vijana Duniani, itaadhimisha Mkutano wa Miito kwa sababu ya SViD huko Lisbon 2023. Itakuwa Jumatatu ijayo, Agosti 7 4:30 p.m (GMT +1) kwenye Paseo Marítimo ya Algés. Watashiriki zaidi ya vijana 75,000 kutoka sehemu mbalimbali za dunia, watakaokuwa wamemsindikiza Baba Mtakatifu Fransisko katika wiki ya maadhimisho ya

Hatua mpya katika awamu ya Roma ya Mchakato wa Kutangazwa Mwenye heri kwa Marta Obregón

Siku ya Ijumaa, tarehe 5 Mei 2023, katika Idara ya Michakato ya Watakatifu ya Vatikano, kumekuwa na tukio la Ufunguzi wa masanduku ya Maandiko ya mchakato wa kijimbo wa kutangazwa Mwenye heri na Mtakatifu kwa Marta Obregón kwa njia ya kifo cha kishahidi. Limekuwa tukio rahisi lakini lenye adhama, la kupendeza na lenye hisia kubwa. Hatua hii inaashiria endeleo la utafiti wa kina unaotekelezwa katika awamu hii ya pili. Walihudhuria

María Ascensión Romero, mjumbe wa Idara ya Uinjilishaji

Uteuzi wa Wajumbe wa Idara ya Uinjilishaji. Kitengo cha maswala ya msingi ya uinjilishaji duniani. Papa Fransisko anawakaribisha Kikundi cha Kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato tarehe 20 Septemba 2019 Baba Mtakatifu, Papa Fransisko ameteua leo tarehe 25 Aprili 2023 Wajumbe wa Idara ya Uinjilishaji, Kitengo cha Maswali ya Msingi ya Uinjilishaji Duniani, kwa muhula wa miaka 5. Miongoni mwao, pamoja na makardinali kumi kutoka sehemu mbalimbali za dunia, maaskofu wakuu

Hija Farlete (Zaragoza – Hispania)

Kumgundua Charles de Foucauld katika Mapango ya Farlete “Huko nilikaa siku tatu katika pango, pango la Mtakatifu Kaprasi, peke yangu, bila kula, nikimsoma Charles de Foucauld, ambaye alinipa tia namna ya kuishi katika uwepo wa Bwana.” Kiko, katika Kuishi Pamoja ya Mwanzo wa Mwaka 2016-2017 Kabla ya kuanza safari kupitia Ulaya, na kwa kuitayarisha, Padre Aguilar alitaka kumpe-leka Kiko kwenye jangwa la Los Monegros, huko Farlete (mkoa wa Zaragoza), ambapo

Hija Zaragoza (Hispania)

Bikira wa Pilar Mnamo Januari 2, mwaka 40, ukingoni mwa Mto Ebro, Bikira Maria, ambaye bado alikuwa anaishi Palestina, alikuja Zaragoza katika mwili wake halisi ili kumfariji mtume Yakobo, aliyesindikizwa na kikundi kidogo cha waongofu, waliokuwa wamehubiri siku nzima. Maria aliwaachia nguzo ya yaspi ambapo Wakristo wa karne ya kwanza walijenga, kama ukumbusho, kanisa dogo ambalo limepanuliwa na kurekebishwa kwa karne nyingi. Wanasema kwamba Papa (Mtakatifu Yohane Paulo II) alipokuja