Hija Farlete (Zaragoza – Hispania)

Kumgundua Charles de Foucauld katika Mapango ya Farlete “Huko nilikaa siku tatu katika pango, pango la Mtakatifu Kaprasi, peke yangu, bila kula, nikimsoma Charles de Foucauld, ambaye alinipa tia namna ya kuishi katika uwepo wa Bwana.” Kiko, katika Kuishi Pamoja ya Mwanzo wa Mwaka 2016-2017 Kabla ya kuanza safari kupitia Ulaya, na kwa kuitayarisha, Padre Aguilar alitaka kumpe-leka Kiko kwenye jangwa la Los Monegros, huko Farlete (mkoa wa Zaragoza), ambapo

Hija Zaragoza (Hispania)

Bikira wa Pilar Mnamo Januari 2, mwaka 40, ukingoni mwa Mto Ebro, Bikira Maria, ambaye bado alikuwa anaishi Palestina, alikuja Zaragoza katika mwili wake halisi ili kumfariji mtume Yakobo, aliyesindikizwa na kikundi kidogo cha waongofu, waliokuwa wamehubiri siku nzima. Maria aliwaachia nguzo ya yaspi ambapo Wakristo wa karne ya kwanza walijenga, kama ukumbusho, kanisa dogo ambalo limepanuliwa na kurekebishwa kwa karne nyingi. Wanasema kwamba Papa (Mtakatifu Yohane Paulo II) alipokuja

Hija Barbastro (Huesca – Hispania)

Barbastro na Mashahidi wake Wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania, Kanisa Katoliki lilipitia madhulumu makubwa, watu 10,000 waliuawa kwa imani yao. Barbastro, licha ya udogo wake, lilikuwa jimbo lenye mashahidi wengi zaidi katika Hispania nzima, 88% ya wakleri. “Hispania imetoa “Kozi” za Ukristo, Opus Dei, Njia ya Neokatekumenato na chochote unachotaka, unajua kwa nini? , kwa sababu ilitamalaki vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo mapadri zaidi ya

Mpito kwa Baba wa Benedict XVI – Ujumbe kutoka Kiko Argüello

UJUMBE WA KIKO KWA JUMUIYA ZA NEOKATEKUMENATO Madrid tarehe 31 Desemba 2022 Kumbukumbu ya Mtakatifu Silvester, Papa Ndugu wapendwa: Tumepokea hivi punde habari za kwenda kwa Baba kwa Papa Mstaafu Benedict XVI. Nakwakumbusha kwamba, tangu alipokuwa Profesa, na baadaye akiwa Mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Imani, na kisha akiwa Papa, tumekuwa daima na shukrani ya pekee na upendo kwake; baada ya Papa Mtakatifu Paulo VI na Papa Mtakatifu Yohane

Sala kwa ajili ya Papa Benedict XVI

Madrid, 29 Desemba 2022 Ndugu wapendwa: Papa Fransisko, kwenye hadhira yake kuu Jumatano iliyopita, ameliomba Kanisa zima la Ulimwengu kuinua maombi kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict XVI, ambaye afya yake imedhoofika sana katika siku za hivi karibuni. Sisi ndugu wa Njia ya Neokatekumenato tunajiunga na ombi hili. Ni kiasi gani tunachopaswa kumshukuru Papa Benedict kwa upendo wake kwa ajili ya Njia, uliodhihirishwa katika matukio mengi mbali mbali! Tusali pamoja

Hija Fuentes de Carbonero el Mayor (Segovia – Hispania)

Kanisa la Fuentes de Carbonero Mahali pa kuhiji na kuadhimisha, ushuhuda wa historia ambayo Mungu hufanya pamoja nasi. «Nilishangaa sana kwamba wakati nyumba zote katika kijiji hicho ziliharibika, kitu pekee kilichobaki kikisimama katika kijiji hicho kilichotelekezwa kilikuwa kanisa, na kanisa ambalo limejaa maskini.Hapa tulisherehekea Mkesha wa Pasaka na ndugu wa vibandani na wale wa jumuiya ya kwanza ya Madrid. Hatukuwa na umeme; Tulijiangazia na nuru ya mshumaa mkubwa wa zamani

Maoni mubashara katika hafla ya ufunguzi wa mchakato ya Kutangazwa kuwa Mwenye Heri kwa Carmen Hernández

Maoni ya Kiko Argüello Jioni njema kwenu nyote, Namsalimu Mha. Carlos Osoro, Kardinali-Askofu Mkuu wa Madrid. Mwadhama Kardinali Antonio Maria Rouco, Askofu Mkuu Mstaafu wa Madrid. Kardinali Paolo Romeo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Palermo. Maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi waliopo hapa. Mama Mkuu wa Wamisionari wa Kristo Yesu na washauri wake. Ni furaha gani unayotupatia uwepo wenu katika hafla hii, madada! Mkuu wa Chuo, Pd. Daniel Sada, Wakuu wa